Viashirio ya tahadhali ya udanganyifu wa ajira

Zifuatazo ni baadhi ya mifano ya udanganyifu wa ajira ambayo inakiuka taratibu za VFS Global na maadili yake ya kazi:

  • Barua pepe haitumwi kutoka kwa anwani ya barua pepe ya VFS Global ila kutoka kwa huduma ya barua pepe ya bure kama: Hotmail, Gmail, Outlook, Yahoo, nk. Pia inawezekana kwamba barua pepe inatumwa kutoka kwenye anuani bandia ya barua pepe.
  • Unaombwa kufichua taarifa binafsi au za siri.
  • Unaombwa kufanyiwa usaili kwa njia ya simu au mfumo wa ujumbe wa papo kwa hapo.
  • Unatakiwa kulipa ada / fedha.
  • Umeombwa kujaza nyaraka za uongo za ajira ya kazi kama vile fomu ya maombi ya viza ya ajira, (jina la VFS Global na nembo inaweza kugushiwa / kutungwa na kuwekwa kwenye nyaraka zisizo na mamlaka.
  • Kusisitiza juu ya uharaka.
  • Fedha itaombwa kwa ajili ya kufanya michakato ya upatikanaji wa vibali vya kazi, maombi ya Visa au kadhalika.

Vitendo hivyo huenda vina nia ya kulaghai au kupata taarifa binafsi kutoka kwa wahanga. Shughuli za watu hawa zinahusisha makosa ya jinai na ya kiraia. Wakati VFS Global Inachukua jambo hili kwa umakini na wana haki ya kuwasiliana na vyombo vya sheria vyenye uwezo wa kuchunguza na kushitaki shughuli hizo zinazofanyika kinyume cha sheria, ni vigimu kuwapata watu hawa na kuwafungulia mashtaka.

Hivyo basi, kama utapokea ombi, kwa maandishi au kwa maneno Aidha, kwa ajili ya mahojiano/usaili au kwa kupata ofa ya kazi na unaamini kwamba inaweza kuwa na tuhuma au ulaghai, Tafadhali yapuuzie. Unaweza pia kuthibitisha na VFS Global katika communications@vfsglobal.com

Kama utatambua kwamba kuna udanganyifu unaofanywa, tunahimiza uwasiliane na polisi mahalia / au Mamlaka yoyote husika na pia kutupa sisi habari kwa kuripoti udanganyifu katika acco@vfsglobal.com

Katika hali yoyote VFS Global inaweza kuwajibika au kuwajibika kwa hasara, uharibifu, gharama au usumbufu wowote utakaotokana na watu/shughuli zisizo halali.