Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Kituo cha maombi ya viza

Kituo cha Maombi ya Viza ni nini (Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada)? >

Vituo vya Maombi ya Viza za Kanada vimeanzishwa ili kutoa msaada wa kiutawala kwa wateja kwaajili ya kufanikisha kuwasilisha maombi ya viza za muda mfupi (viza za matembezi, vibali vya masomo na kazi) pamoja na hati za kusafiria kwa wakazi wa kudumu wa Kanada katika ofisi za IRCC duniani kote

 

Ni nani mkandarasi wa CVAC inchini Nairobi >

VFS Global ni kampuni binafsi iliyo ithinishwa na Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada kuendasha Kituo cha maombi ya viza za Kanada inchini

 

Je! Naweza panga miada kwa Dharura?>

Waombaji wanaoomba miadi ya dharura kwa madhumuni ya kusajili bayometriki wanaweza kufanya hivyo kwa kuonyesha dhamana itakayofaa kuwasilishwa wakati wa appointmenti. Dhibitisho inayofaa inaweza kujumuisha daftari au nyaraka zingine kutoka kwa afisa. Tafadhali kumbuka kuwa uthibitisho huu unahitaji tu kuwasilishwa na hautakusanywa na Kituo cha Maombi ya Viza, na kwamba hii itatoa miadi ya dharura ya bayometriki lakini haitaathiri wakati wa tathmini wa IRCC kwa ombi lako. Kwa habari yoyote zaidi au maswali, Kituo cha Mawasiliano kinaweza kukusaidia.

 

Tafadhali Bonyeza hapa Kuweka Miadi

 

Mchakato wa maombi

Niwasilishe wapi maombi yangu ya viza?

Unaweza kuwasilisha maombi yako ya viza katika Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada. Maombi yanaweza pia kuwasilishwa kwenda ofisi za IRCC kwa kutumia mfumo wa kimtandao wa maombi ya viza wa IRCC(E-Apps)

 

Je mtu mwingine anaweza kuwasilisha maombi kwa niaba yangu?

Unaweza kuteua muwakilishi akuwasilishie maombi kwa niaba yako Ili kufanya hivyo, tafadhali jaza Fomu ya Kutumia Uwakilishi na/ au Fomu ya Ridhaa ya VFS Global, kumruhusu muwakilishi awasilishe au achukue kifulushi cha maombi yako/ bahasha yenye majibu kwa niaba yako.

 

Je nitatakiwa kwenda mwenyewe kutoa alama za vidole na picha kila ninapofanya maombi ya viza?

Iwapo unaomba viza ya muda mfupi, masomo au idhini ya kufanya kazi, itasajili bayometriki mara moja katika kila miaka 10.

Ili kujua kama unahitajika kutoa biometriki, tafadhali tembelea http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometric.asp.

 

Mara ninapotoa alama za vidole na picha, alama zangu za vidole zitakuwa halali kwa muda gani?

Kuanzia Julai 31, 2018, biometriki zinadumu kwa miaka kumi. Kama umetoa alama zako za vidole na picha zamani, zitaendelea kutumika kwa miaka kumi tangia siku zilipochukuliwa. Muda wa matumizi ya Viza au kibali hauwezi kuzidi muda wa matumizi ya alama zako za vidole na picha. Waombaji wa Makazi ya Kudumu watatakiwa kutoa alama za vidole na picha kila wanapowasilisha maombi.

Alama zako za vidole zitafutwa moja kwa moja kama utapewa Uraia wa Kanada ndani ya kipindi cha miaka 10.

 

Je natakiwa kutoa buometriki kwa ajili ya maombi yangu ya viza?

Ili kujua kama unahitajika kutoa biometriki, tafadhali tembelea http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometric.asp. 

Je ni lazima niweke miadi kwajili ya kutoa alama zangu za vidole na picha katika Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada?

Kuanzia tarehe 02 Novemba 2019, miadi ni lazima kwaajili ya kutoa alama za vidole na picha katika Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada nchini Tanzania.

 Ili kujua kama unahitajika kutoa biometriki, tafadhali tembelea http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometric.asp.

Tafadhali tambua kwamba, kwaajili tu ya kupanga miadi, VFS Global itachukua taarifa binafsi toka kwa mteja Fomu ya ridhaa kwa ajili hiyo itatakiwa toka kwa mwombaji wa viza.

 

Nitalipiaje ada za Serikali ya Kanada kwaajili ya maombi yangu ya viza?

Ada za Serikali ya Kanada zinaweza kulipwa mtandaoni kupitia tovuti ya IRCC kwa kadi ya malipo au mkopo kutokea Benki ya kikanada kwa kutumia INTERAC® Online na zilizosajiliwa kufanya malipo ya mtandaoni kupitia tovuti ya benki. Kulipia ada za serikali ya Kanada mtandaoni tafadhali bofya hapa

 

Ninafanyaje malipo ya gharama za viza na huduma za CVAC?

Kwa maagizo kamili kuhusu Serikali ya Canada malipo ya ada na malipo ya Kituo cha Maombi ya Visa tafadhali bonyeza hapa

hiari

• Binafsi – Kupitia Mpesa

• Ombi la kutumwa na Courier/posta – Ada inaweza kulipwa kwa uhamisho kwa benki kwa "VFS Nairobi Limited" kwa shilingi ya Nairobi tu

Ufuatao ni muongoza wa malipo ya uhamisho kwa benki

Akaunti ya VFS Global Nairobi limited

Jina la akaunti: VFS (Nairobi) Limited- Canada Holdings Nchi: Nairobi Fedha: Nairobi Shilling Jina la Benki: Barclays Bank Tawi: Barclays Plaza Mtaa: Loita Street - Nairobi Nambari ya akaunti. 2037342214 Nambari ya IBAN. 2037342214 Nambari ya SWIFT: BARCKENX Nambari ya Chips UID/Sort code: 03

Maelezo ya akaunti ya benki

Benki ya mawasiliano: Barclays New York Jiji/mtaa: New York Nchi: USA Nambari SWIFT: BARCUS33

Kwa taarifa kamili juu ya malipo ya ada Serikali ya Kanada na Kituo cha Maombi ya viza, tafadhali bonyeza hapanyeza hapa

 

Nini kitatokea nikiisha wasilisha maombi yangu ya viza?

Ukishawasilisha maombi yako katika Kituo cha Maombi ya Viza, mfanyakazi wa Kituo cha Maombi ya Viza atakagua ukamilifu wa maombi yako kulingana na vigezo vya IRCC na watawaslisha maombi yako kwa niaba yako siku ya kazi inayofuata.

Mara maamuzi juu ya maombi yako yakiishafanywa, ofisi za viza zitarudisha kwa usalama pasipoti yako kwa katika Kituo cha Maombi ya Viza, ambao watakutaarifu kwa njia ya mawasiliano utakayoipendelea wewe. Taarifa itatolewa pia katika Mfumo wa Ufuatiliaji wa Maombi Mtandaoni, kukujulisha kwamba majibu ya maombi yako yapo tayari kurejeshwa. Majibu ya maombi yako yatarudishwa kwako kwa njia ya urejeshaji utakayopendelea.

 

Ninahitaji Viza ya aina gani?

Aina ya viza unayohitaji itategemea na dhumuni la safari yako ya Kanada. kwa taarifa zaidi kuhusu aina za viza tafadhali angalia taarifa za kina zilizomo katika tovuti IRCC

 

Nianawezaje kufuatilia maendeleo ya maombi yangu?

Maendeleo ya maombi yako yanaweza kufuatiliwa kwa urahisi kwa kubofya “Fuatilia Maombi yako”

 

Ninawezaje kuipata pasipoti yangu?

Kupata pasipoti yako (zako), una machaguo mawili:

1. Kuchukua pasipoti yakow ewe mwenyewe toka Kituo cha Maombi ya Viza au,

2. Kuomba pasipoti yako irudishwe kwa njia ya kuria

Tafadhali tambua kuwa kutakuwa na ada za huduma tajwa hapo juu. Ada za Kuria zinapohusika ni tofauti na ada za malipo kwaajili ya Huduma za Kuwasilisha Pasipoti. Taarifa zaidi zinaweza kupatikana katika ukurasa wa ada za huduma.

 

Ninahitaji kuwa na nyaraka gani ili niweze kupata pasipoti yangu?

Kama unachukua paspoti yako wewe mwenyewe, ni lazima uje na:

1. Nakala ya ukurasa wenye picha wa pasipoti yako uliopigwa muhuri.

2. Risiti halisi iliyotolewa na Kituo cha Maombi ya Viza

3. Kitambulisho cha kiserikali

 

Mchakato wa viza utachukua muda gani?

Kwa muda wa mchakato wa maombi wa hivi karibuni, tafadhali tembelea tovuti ya Ofisi ya Viza

 

Je nitatakiwa kuhudhuria kwenye usahili katika Ofisi za Viza?

Ofisi ya IRCC inaweza kukuhitaji uhudhurie kwenye usahili katika Ofisi za Viza na utataarifiwa pia kwa taarifa katika Mfumo wa Kufuatilia Maombi Mtandaoni.

 

Niwasiliane nan ani kwa maelezo zaidi?

Unaweza kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kinachoendeshwa na Kituo cha Maombi ya Viza (Tafadhali rejea kitufe cha “Wasiliana Nasi” kilicho kushoto mwa ukurasa huu)

 

Huduma gani za ziada zipo kwaajili yangu?

Kituo cha Maombi ya Viza kinatoa aina mbalimbali za huduma kwa manufaa yako na kurahisisha ufanyaji wa maombi ya Viza kama vile kutoa nakala (fotokopi), kuria, msaada wa kujaza fomu. Kwa maelezo kamili na gharama za huduma hizo tafadhali rejea “Orodha ya Huduma na Ada za Huduma”

 

Ninampango wa wa kwenda Kanada kusoma kwa kipindi kisichozidi miezi sita lakini ninaweza kuhitaji kuongeza muda wa masomo. Je niwasilishe aina gani ya maombi?

Tafadhali rejea: https://www.canada.ca/en/immigration-refugees-citizenship/services/study-canada/study-permit/eligibility.html

Nyaraka

 

Ni nyaraka gani ninazotakiwa kuwa nazo kwa ajili ya kuomba viza?

Nyaraka zinazohitajika zinategemea kusudi la safari yako. Tafadhali rejea kwenye sehemu ya kushoto ya ukurasa wa Kuandaa maombi yako na fuata viunganisho husika vilivyotolewa au tembelea wavuti ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada.

Je Ofisi za Viza zinaweza kuniomba nyaraka au taarifa za ziada?

Ndio, Ofisi za Viza zinawezakukuhitaji uwasilishe nyaraka za ziada Taarifa itawekwa kwenye Mfumo wa Ufuatiliaji Maombi Mtandaoni na itafuatiwa na taarifa kwa njia ya barua pepe kuhakikisha kwamba umepokea maelekezo na taarifa. Halafu utaombwa kuwasilisha nyaraka za ziada kwenye Kituo cha Maombi ya Viza amabo wataziwasilisha Ofisi za Viza kwa niaba yako. 

 

NNingependa kwenda Kanada kama mwanafunzi. Ni gharama gani zinahitajika kwa ajili ya masomo?

Gharama zinazotakiwa kwa ajili ya wanafunzi zinategemea muda utakaokaa Kanada. Tunakushauri utembelee wavuti ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada ili kupata taarifa za hivi karibuni na kuhakikisha kuwa nyaraka ulizonazo zinakidhi vigezo wakati wa kupeleka ombi lako kwenye Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada cha Nairobi.

Kama wewe ni mwanafunzi unayekwenda kusoma kwenye Jimbo la Quebec, unatakiwa kusoma pia maelezo kwenye wavuti ya Uhamiaji-Quebec