Sera za faragha na ukanushi

Kano la Dhima

TMasharti yafuatayo yanawahusu Waombaji wa Viza wanaotumia au wanaopanga kutumia Huduma zitolewazo na Kituo cha Viza za Kanada wanaofika wenyewe ofisini au wanaotuma maombi yao.

Kampuni ya VFS Worldwide Holdings Ltd (ambayo hapa itajulikana kama “VFS”) ni mtoa huduma wa mamlaka ya Uhamiaji, Ukimbiza na Uraia Kanada, (IRCC”). Katika utekelezaji wa jukumu hilo, VFS Inaendesha Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada kwa kupewa mamlaka na IRCC ya kufanya kazi za kiutawala za IRCC kwa ajili ya maombi ya viza na vibali vya muda mfupi na maombi ya nyaraka za kusafiria kwa ajili ya wakaazi wa kudumu wa Kanada. Waombaji wanakubali na wanatambua kwamba gharama zinazotozwa na VFS kwa ajili ya huduma wanazopewa hazitarejeshwa, kwa kuzingatia kigezo chochote.

Waombaji wanatambua kwamba Ofisi inayohusika na Viza za Kanada inayo haki ya kuwataka waombaji wawasilishe nyaraka zaidi au wafanyiwe usaili ili kufanya maamuzi kuhusu maombi yao ya viza.

CVAC haitawajibika wala kuwa na dhamana na:

 1. Matokeo ya ombi lolote la viza.
 2. Isipokuwa pale ilipotajwa katika mkataba huu, VFS, haitawajibika na uharibifu, upotevu au madhara ya aina yoyote ile yanayotokana na ucheleweshaji wa mchakato au kukataliwa kwa ombi lolote la viza.
 3. Pamoja na kuwa na tahadhari kubwa katika kushughulikia nyaraka za maombi, zikiwemo pasi za kusafiria, CVAC, haitawajibika (isipokuwa pale ilipotajwa katika makataba huu) chini ya mkataba, kwa namna yoyote, kwa uharibifu, upotevu au madhara ya aina yoyote hata kama yanatokana na:

 1. Ushughulikiaji wa pasi za kusafiria na nyaraka zingine unaofanywa na CVAC na wakandarasi wengine wadogo;
 2. Huduma zozote ya ongezeko la thamani zinazotolewa na waombaji;
 3. Majaliwa ya Mwenyezi Mungu;
 4. Ajali ama wizi wa aina yoyote;
 5. Mazingira mengine yoyote nje ya uwezo wa CVAC na wakandarasi wengine wadogo.

Endapo pasi ya kusafiria imepotea ama kuharibika wakati wa kusafirishwa au ikiwa mikononi mwa Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada / wakandarasi wadogo, wajibu wa VFS, na / au Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada / wakandarasi wadogo ni ule wa kurejesha gharama rasmi zinazohitajika na mamlaka husika kwa ajili ya kupata pasi mpya ya kusafiria kulingana na taratibu za kiofisi tu. VFS, na / au Kituo cha Viza za Kanada / Wakandarasi wadogo hawatahusika ama kuwajibika na upotevu ama uharibifu wa pasi ya kusafiria au nyaraka zilizoambatishwa.

Gharama kwa huduma zinazotolewa na VAC na kuorodheshwa kwa orodha ya malipo zinazolipwa na waombaji wa viza hazitarejeshwa.

VFS imeweka viunganisho na wavuti zingine ambazo waombaji wangependa kuzitembelea. VFS haizisomi wavuti hizo wala kudhibiti mambo yaliyomo humo. Hivyo, VFS haitawajibika kwa namna yoyote endapo mwombaji atatembelea wavuti hizo na kupata huduma huko. Mara waombaji wanapoingia kwenye wavuti nyingine, wanawajibika kufuata vigezo na masharti ya mtandao husika. Ni muhimu pia kutambua kwamba hakuna mwajiriwa / mkandarasi mdogo wa VFS mwenye mamlaka ya kubadilisha, kurekebisha ama kuongeza vipengele vya mkataba huu.

Hata hivyo, katika hali yoyote ile, Masharti haya yatasimamiwa na sheria za Kenya na migogoro yoyote inayotokana na masharti haya itapelekwa kwenye Mahakama za nchi ya Kenya

 

Sera ya Taarifa Binafsi

Mipaka ya Kiutendaji

VFS Global Services (ambayo itajulikana kama “VFS”) ni mshirika wa Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC), Kanada na ameidhinishwa kufanya shughuli za kiutawala zinahusiana na maombi ya viza za muda mfupi, vibali vya ukaazi, nyaraka za kusafiria. Maelezo kuhusu taarifa binafsi yanafafanua namna VFS inavyokusanya, kutumia, kutoa na kusimamia taarifa binafsi za watu (ambao katika mkataba huu watajulikana kama “Waombaji”) wanaoomba viza na vibali vya ukaazi na kuziwasilisha kwa mamlaka husika kwa kusudi lililofafanuliwa hapa chini.

Taarifa binafsi zinaweza kukusanywa kwa lengo la:

 • Kushughulikia maombi ya viza za muda mfupi, kibali cha ukaazi na nyaraka za kusafiria;
 • Kutoa majibu kuhusu mchakato wa maombi;;
 • Kufuatilia maombis; na
 • Kujibu maswali ya waombaji (yaani, “Huduma”)

VFS hukusanya taarifa binafsi za waombaji kwa ajili ya kutoa huduma hizo tu. Taarifa zako binafsi hazikusanywi kwa niaba ya Serikali ya Kanada, lakini taarifa hizo na nyaraka zitatolewa kwa Serikali ya Kanada kwa ajili ya kurahisisha mchakato wa maombi ya viza. Utoaji wa taarifa binafsi kwa VFS ni wa hiari. Hata hivyo, inabidi kutambua kwamba kukataa kutoa taarifa binafsi kunaweza kunaweza kupunguza uwezo wetu wa kutoa huduma zilizooombwa. Taarifa binafsi hukusanywa moja kwa moja kutoka kwa wafanyakazi wa wakala wa huduma za usafiri au mwakilishi yeyote aliyeidhinishwa. Mwombaji ni lazima atoe ridhaa kwa kutumia fomu ya ridhaa kulingana na aina ya ridhaa; yaani ya moja kwa moja ama isiyo ya moja kwa moja.

Mchakato wa maombiing: AKatika fomu ya maombi ya viza, waombaji wanaweza kuambiwa watoe taarifa binafsi kama vile jina, picha, anwani, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya simu, taarifa zinazohusu pasi ya kusafiria, cheti cha kuzaliwa, kipato, hali ya uraia, hali ya ndoa na historia ya ajira, makosa ya jinai na elimu. Taarifa hizi binafsi zinakusanywa ili kuiwezesha Serikali ya Kanada na / au Ofisi husika zinazoshughulikia Viza za Kanada nyaraka kushughulikia maombi ya viza na vibali vya ukaazi. Taarifa binafsi zitatumika pia kuirejesha pasi ya kusafiria na nyaraka za mwombaji mara baada ya kukamilisha mchakato wa viza kwenye Ofisi ya Viza ya Kanada kulingana na utaratibu ulioanishwa wakati wa kuwasilisha ombi.

 

Maswali ya Waombaji:: Baadhi ya taarifa binafsi kama vile jina la ukoo, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya simu, anwani ya mtaa, anwani ya barua pepe, tarehe ya maombi na utambulisho binafsi zinaweza kupatikani endapo utatupigia simu na kutuuliza kitu ama kutoa maoni yako. Tafadhali, tambua kwamba mawasiliano ya barua pepe yanaweza yasiwe salama. Waombaji wasitoe taarifa za siri kama vile nambari ya pasi ya kusafiria kupitia mawasiliano ya barua pepe au simu. Tunashauri Waombaji kutoweka wazi aina ya huduma wanayoiomba kupitia barua pepe.

 

Utoaji wa Taarifa Binafsi:: VFS haitazifanyia biashara, kuziuza ama kuzituma taarifa zako binafsi tofauti na ilivyobainishwa katika mkataba huu. Taarifa zako binafsi zitatumiwa kwa makusudi yaliyotajwa katika mkataba huu. VFS inaweza kulazimika kisheria kutoa taarifa za siri ili kutekeleza amri ya mahakama, kesi inayoendelea mahakamani, au mchakato mwingine wa kisheria unaoitaka VFS kutoa taarifa au kutekeleza haki za kisheria ama kujitetea dhidi ya madai ya kisheria, upelelezi wa makosa ya jinai, masuala ya kimahakama, usalama wa taifa, upelelezi, kubaini makosa, uendeshaji wa mashitaka ya jinai.

 

Upelekaji wa Taarifa Kanada:: Taarifa binafsi zinazokusanywa na VFS zitapelekwa ofisi ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC), iliyopo nchini Kanada, kwa lengo la kushughulikia maombi na malengo mengine ya utoaji wa Huduma. Taarifa zilizo katika mfumo wa kieletroniki zitabakia kwenye hifadhi ya data ya VFS katika vituo vya data vilivyopo Kanada.Taarifa za alama za vidole zinazokusanywa na VFS zitapelekwa moja kwa moja IRCC nchini Kanada. Tafadhali, tambua kwamba taarifa binafsi zitajumuishwa kwenye hifadhi kuu ya taarifa binafsi inayodhibitiwa na Ofisi ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada.(IRCC)

 

Mipangilio ya Utoaji wa Huduma: VFS inaweza kupeleka (ama kuzitoa) taarifa binafsi kwa mtu mwingine anayetoa huduma kwa niaba yetu. Kwa mfano, tunaweza kuwatumia watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi. Taarifa binafsi kama vile jina, anwani, nambari ya simu zinaweza kutolewa kwa watoa huduma za kusafirisha vifurushi. Taarifa binafsi hazitatolewa kwa mtoa huduma za ujumbe mfupi (SMS). Taarifa zako binafsi zinaweza kuhifadhiwa na kushughulikiwa na watoa huduma nje ya Kanada. Watoa huduma hupewa taarifa wanazozihitaji katika utekelezaji wa majukumu yao na hatuwaruhusu kutumia ama kuzitoa taarifa binafsi kwa malengo yao.

 

Kuki

Kuki ni mafaili ama taarifa ambazo zinaweza kuhifadhiwa katika mfumo wa kompyuta au kifaa chenye intaneti unapotembelea wavuti ya VFS. Unapoingia kwenye wavuti ya VFS, unaridhia matumizi yetu ya kuki. Kama hujaridhia basi usitumie wavuti yetu. Kama kuki hazifanyi kazi zinaweza kuathiri mazoea ya watumiaji wa wavuti yetu. VFS hutumia kuki kurahisishai matumizi ya wavuti. Hatuwezi kukutambua wewe binafsi kupitia taarifa hizi.

 • Wavuti ya VFS huweza kuonyesha baadhi ya vitu amabvyo haiwezekani kuvionyesha bila kutumia kuki.
 • Kuki husaidia kuwatambua waombaji au watumiaji wa wavuti na kuwafanya waendelee kubakia ndani ya wavuti.
 • Kuki nyingi hutokea ukiwa mtandaoni tu na hufutika zenyewe katika kifaa cha kuhifadhia data cha mtumiaji mara baada ya kutoka kwenye intaneti. Baadhi ya kuki hubakia kila unapotembelea wavuti zetu.
 • Mwombaji / mtumiaji wa wavuti ana uhuru wa kukataa kuki endapo ukurasa husika unatoa uwezekano huo, ingawa kufanya hivyo kunaweza kusababisha matatizo katika utumiaji wa wavuti.
 • Mwombaji / Mtumiaji wa wavuti anaweza kukutana na kuki anapotumia viungovingine ama katika kurasa fulani za wavuti ambazo hazipo chini ya udhibiti wa VFS kama vile viungokwenye wavuti ya IRCC na / au viunganisho vingine vilivyoidhinishwa na IRCC / VFS na wakandarasi wake wadogo hawaruhusu spam. Mtumiaji au watumiaji hawaruhusiwi kuongeza, kurekebisha, kubadilisha mwonekano, kuiba, au kutumia vibaya wavuti ya VFS ama taarifa zilizomo ndani ya wavuti hiyo. Ili kutoa taarifa kuhusu spam au ujumbe wa vichekesho wa barua pepe, tuma ujumbe wa barua pepe kwa communications@vfsglobal.com
 • Mwombaji / mtumiaji wa wavuti haruhusiwi kutumia vyombo vya mawasiliano vya VFS ama ukurasa wa wavuti kutuma spam au taarifa zinazovunja makubaliano yetu na mtumiaji. VFS huchuja na kuskani ujumbe kwa ajili ya kuondoa virusi ama taarifa ambazo haziruhusiwi kabla ya kuutuma ujumbe husika. VFS haihifadhi ujumbe wa barua pepe kwa muda mrefu. VFS haikodishi wala kuuza anwani za barua pepe kwa mtu wa tatu.

Usalama

VFS imechukua hatua zenye lengo la kusaidia kulinda taarifa binafsi zinazodhibitiwa nasi. Hatua za kiutawala, kiufundi, kimazingira na kiitaasisi zimechukuliwa ili kudhibiti upatikanaji, utumiaji, ubadilishaji na utoaji wa taarifa binafsi zilizo chini ya udhibiti wetu.

 

Kuhifadhi & Kuharibu Taarifa

Nyaraka za maombi zilizokusanywa kutoka kwa waombaji hazitanakiliwa ama kuhifadhiwa na VFS. Karatasi yoyote, nakala ngumu, fomu, ama kumbukumbu nyingine zozote zenye taarifa binafsi zitaharibiwa kwa njia salama ndani ya siku (30) baada ya pasi ya kusafiria kurejeshwa kwa mwombaji.

Hii ni kwa ajili ya kuwasaidia waombaji endapo watawasiliana nasi kwa ajili maswali yanayohusiana na mchakato mzima. VFS hutumia njia salama za kutupa ama kuharibu taarifa binafsi au kifaa kilichotumika kuzihifadhi taarifa hizo. Wakati wa kuzitupa au kuziharibu taarifa binafsi, VFS huchukua hatua muafaka za kuzuia watu wasiohusika kuvitumia vifaa ama vyombo vilivyotumika katika kuhifadhia taarifa binafsi (kama vile makabati ya mafaili, kompyuta, disketi na mikanda ya audio). Hatu zinazochukuliwa ni pamoja na kuondoa au kufuta taarifa zilizohifadhiwa ama kuzuia zisitumiwe na watu wasiohusika.

 

Masuala ya Kisheria

VFS na watoa huduma wake wanaweza kuzitoa taarifa zako binafsi kwa ajili ya kibali cha kukamatwa, maulizo au amri nyingine ya kisheria. Tunaweza pia kutoa taarifa zako kwa chombo cha upelelezi endapo kuna uvunjifu wa mkataba au sheria, au kulingana na matakwa ya sheria husika. VFS inaweza pia kutoa taarifa zako binafsi kwa ajili ya ushahidi ama utetezi katika madai ya kisheria kulingana na matakwa ya sheria husika.

 

Viunganisho Kwenye Wavuti Zingine

Wavuti yetu inaweza kukuunganisha na wavuti zingine amabazo hazimilikiwi wala kuendehswa na VFS kama vile wavuti za IRCC au wavuti zingine zilizoidhinishwa na IRCC, n.k. Tunaziweka wavuti hizi kwa ajili ya kukusaidia na hii haimainishi kuwa VFS ina mahusiano yoyote na wavuti hizo. VFS, maafisa, wafanyakazi na mawakala wake hawatawajibika kwa namna yoyote na wavuti zingine na habari zilizomo katika wavuti hizo kwani hakuna habari yoyote iliyomo humo iliyoidhinishwa na VFS na washirika wake. Wavuti zilizounganishwa na VFS zinajitegemea na zina sera, maelezo na masharti yake ya matumizi ya taarifa binafsi na tunakushauri uyaelewe vizuri yote haya. Hatuna udhibiti wa aina yoyote wa wavuti hizo; hivyo hatuwajibiki na matumizi ya taarifa binafsi yanayofanywa na wavuti hizo.

 

Haki ya Kuzipata na Kuzitumia Taarifa zako Binafsi

Una haki ya kuzitumia na kuyarekebisha makosa yaliyomo katika taarifa zinazokuhusu. Unaweza pia kuomba kuzitumia, kubadilisha au kufanya marekebisho ya taarifa zako binafsi kwa ujumbe wa barua pepe au kwa kutuandikia kupitia taarifa za mawasiliano zilizotolewa hapa chini. VFS haitawajibika na ukweli au usahihi wa taarifa zinazotolewa na Mwombaji. Ni wajibu wa Mwombaji kuhakikisha kuwa taarifa zote anazozitoa kwa VFS ni sahihi.

 

Haki ya Kujitoa (Kuondoa Ridhaa)

VFS inaheshimu maisha yako binafsi na inakupa uhuru wa kukataa kutoa taarifa binafsi zinazotakiwa kuwasilishwa. Unaweza kubatilisha ridhaa yako uliyoitoa mwanzo. Hata hivyo, uwajulishe VFS kuhusu uamuzi huo kwa maandishi. Baada ya mwombaji kubatilisha ridhaa yake, VFS haitaweza kuendelea kumpa huduma za kiutawala ya VAC. Mwombaji anaweza kuwasilisha ombi lake la viza moja kwa moja kwenye ofisi ya IRCC ama ofisi ya viza iliyopo katika nchi husika.

 

Mabadiliko ya Sera ya Taarifa Binafsi

Tafadhali, tambua kwamba Sera ya Taarifa Binafsi inaweza kubadilishwa baada ya muda fulani na tunawashauri waombaji kuitembelea wavuti yetu ili kupata taarifa kuhusu mabadiliko hayo.

 

Wasiliana nasi

Endapo una maswali yoyote kuhusu Sera yetu ya Taarifa Binafsi au namna tunavyoendesha shughuli zetu, unaweza kuandika kwa privacy@vfsglobal.comili kupata maelezo zaidi.

 

Malalamiko na maswali

Endapo unadhani kwamba VFS haijafuata Sera ya Taarifa Binafsi, tafadhali tujulishe kwa ujumbe wa barua pepe kwenye privacyofficer@vfsglobal.com na tutafanya jitihada zote na kuchukua hatua zozote tunazoweza kulishughulikia suala hilo kwa haraka.

 

Unaweza kupeleka malalamiko yako kuhusu mfumo wa usimamizi wa taarifa binafsi kwa afisa wa taarifa binafsi, kwenye privacyofficer@vfsglobal.com.Pia una haki ya kuelekeza malalamiko kwa Ofisi ya Tume ya faragha ya Canada hukohttps://www.priv.gc.ca/en/

 

 

Jitahadhari na matoleo ya kazi ya utapeli

Ajira za ulaghai / Ofa za kazi

Imekuja taarifa ya tahadhari kwa VFS Global kwamba, kuna watu binafsi wanajifanya wenyewe kama wajumbe wa VFS Global au wawakilishi wamewasiliana na watu kutoa fursa za udanganyifu / za uwongo, kwa kusudi la kuiba habari binafsi au kuomba fedha kutoka kwa watu. Tunakuhimiza kuwa muangalifu na kutumia umakini wa ziada wakati unapokea ofa ya ajira, ambayo inahitaji malipo ya ada yoyote / fedha, au ahadi ya kupatiwa visa ya kazi kwa kubadilishana fedha. Programu zinazosema hivyo ni bandia/feki kabisa na sio sahihi. VFS Global si shirika la ajira na haitoi huduma za ajira. Wadangayifu hao hufanya kazi hasa kwa njia ya mtandao, barua pepe, simu nk Tunaonya watu kujihadhari na matukio hayo.

Tafadhali tambua kwamba, VFS Global ni kampuni inayohusika na kusaidia kwenye maombi ya visa na tunafanya kazi na serikali na utawala wa kidiplomasia tuu kutekeleza mahitaji yao ya kiutawala nausaidizi wa maombi ya visa. Si VFS Global wala mawakala wake kwa namna yoyote ile wataomba fedha kutoka kwa watu binafsi ili kuwavutia na fursa za ajira kwenye ofisi za VFS Global ama nje. Ikiwa unapokea ofa yoyote ya kikazi inayoonekana inayotoka VFS Global, ambayo huomba fedha, tambua hizi ni aina za ulaghai.

 

Ishara za onyo la udanganyifu wa ajira

Zifuatazo ni baadhi ya mifano ya udanganyifu wa ajira ambayo inakiuka taratibu za VFS Global na maadili yake:

 • Barua pepe haitumwi kutoka kwa anwani ya barua pepe ya VFS Global lakini kutoka kwa huduma ya barua pepe ya bure kama: Hotmail, Gmail, Outlook, Yahoo, nk. Pia inawezekana kwamba barua pepe inatumwa kutoka kwenye anuani bandia ya barua pepe.
 • Unaombwa kufichua habari binafsi au za siri.
 • Unaombwa kufanyiwa usaili kwa njia ya simu au ujumbe wa papo kwa hapo.
 • Unatakiwa kulipa ada / fedha.
 • Umeombwa kukamilisha nyaraka za uongo za ajira ya kazi kama vile fomu ya maombi ya viza ya ajira, (jina la VFS Global na nembo inaweza kugushiwa / kutungwa na kuwekwa kwenye nyaraka zisizo na mamlaka.
 • Kusisitiza juu ya uharaka..
 • Fedha itatakiwa kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vibali vya kazi, maombi ya Visa au kadhalika.

 

Vitendo hivyo huenda vina nia ya kulaghai au kupata taarifa binafsi kutoka kwa watu watakaoathirika.

Shughuli za watu hawa zinahusisha makosa ya jinai na ya kiraia. Wakati VFS Global Inachukua jambo hili kwa umakini na wana haki ya kuwasiliana na vyombo vya sheria vyenye uwezo wa kuchunguza na kushitaki shughuli hizo zinazofanyika kinyume cha sheria, ni vigimu kuwapata watu hawa na kuwafungulia mashtaka.

Hivyo basi, kama utapokea ombi, kwa maandishi au kwa maneno Aidha, kwa ajili ya mahojiano/usaili au kwa kupata ofa ya kazi na unaamini kwamba inaweza kuwa na tuhuma au ulaghai, Tafadhali yapuuzie. Unaweza pia kuthibitisha na VFS Global katika communications@vfsglobal.com

Kama utakuja kujua kwamba kuna udanganyifu unaofanywa, Tunahimiza uwasiliane na polisi wa mtaa / au Mamlaka yoyote husika na pia kutupa sisi habari kwa kuripoti udanganyifu katikaacco@vfsglobal.com

Katika hali yoyote VFS Global inaweza kuwajibika au kuwajibika kwa hasara, uharibifu, gharama au usumbufu wowote utakaotokana na watu/shughuli zisizo halali.