Jihadhari na kazi za ulaghai

Ajira za ulaghai / Ofa za kazi

Imekuja taarifa ya tahadhari kwa VFS Global kwamba, kuna watu binafsi wanajifanya wenyewe kama wajumbe wa VFS Global au wawakilishi wamewasiliana na watu kutoa fursa za udanganyifu / za uwongo, kwa kusudi la kuiba habari binafsi au kuomba fedha kutoka kwa watu. Tunakuhimiza kuwa muangalifu na kutumia umakini wa ziada wakati unapokea ofa ya ajira, ambayo inahitaji malipo ya ada yoyote / fedha, au ahadi ya kupatiwa visa ya kazi kwa kubadilishana fedha. Programu zinazosema hivyo ni bandia/feki kabisa na sio sahihi. VFS Global si shirika la ajira na haitoi huduma za ajira. Wadangayifu hao hufanya kazi hasa kwa njia ya mtandao, barua pepe, simu nk Tunaonya watu kujihadhari na matukio hayo.

 

Tafadhali tambua kwamba, VFS Global ni kampuni inayohusika na kusaidia kwenye maombi ya visa na tunafanya kazi na serikali na utawala wa kidiplomasia tuu kutekeleza mahitaji yao ya kiutawala nausaidizi wa maombi ya visa. Si VFS Global wala mawakala wake kwa namna yoyote ile wataomba fedha kutoka kwa watu binafsi ili kuwavutia na fursa za ajira kwenye ofisi za VFS Global ama nje. Ikiwa unapokea ofa yoyote ya kikazi inayoonekana inayotoka VFS Global, ambayo huomba fedha, tambua hizi ni aina za ulaghai.;

• Ishara za onyo la udanganyifu wa ajira Zifuatazo ni baadhi ya mifano ya udanganyifu wa ajira ambayo inakiuka taratibu za VFS Global na maadili yake:

• Barua pepe haitumwi kutoka kwa anwani ya barua pepe ya VFS Global lakini kutoka kwa huduma ya barua pepe ya bure kama: Hotmail, Gmail, Outlook, Yahoo, nk. Pia inawezekana kwamba barua pepe inatumwa kutoka kwenye anuani bandia ya barua pepe.

• Unaombwa kufichua habari binafsi au za siri.

• Unaombwa kufanyiwa usaili kwa njia ya simu au ujumbe wa papo kwa hapo..

• Unatakiwa kulipa ada / fedha.

• Umeombwa kukamilisha nyaraka za uongo za ajira ya kazi kama vile fomu ya maombi ya viza ya ajira, (jina la VFS Global na nembo inaweza kugushiwa / kutungwa na kuwekwa kwenye nyaraka zisizo na mamlaka.

• Kusisitiza juu ya uharaka.

Fedha itatakiwa kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vibali vya kazi, maombi ya Visa au kadhalika

Vitendo hivyo huenda vina nia ya kulaghai au kupata taarifa binafsi kutoka kwa watu watakaoathirika. Shughuli za watu hawa zinahusisha makosa ya jinai na ya kiraia. Wakati VFS Global Inachukua jambo hili kwa umakini na wana haki ya kuwasiliana na vyombo vya sheria vyenye uwezo wa kuchunguza na kushitaki shughuli hizo zinazofanyika kinyume cha sheria, ni vigimu kuwapata watu hawa na kuwafungulia mashtaka.

Hivyo basi, kama utapokea ombi, kwa maandishi au kwa maneno Aidha, kwa ajili ya mahojiano/usaili au kwa kupata ofa ya kazi na unaamini kwamba inaweza kuwa na tuhuma au ulaghai, Tafadhali yapuuzie. Unaweza pia kuthibitisha na VFS Global katika communications@vfsglobal.com

Kama utakuja kujua kwamba kuna udanganyifu unaofanywa, Tunahimiza uwasiliane na polisi wa mtaa / au Mamlaka yoyote husika na pia kutupa sisi habari kwa kuripoti udanganyifu katika acco@vfsglobal.com

Katika hali yoyote VFS Global inaweza kuwajibika au kuwajibika kwa hasara, uharibifu, gharama au usumbufu wowote utakaotokana na watu/shughuli zisizo halali.