Fanya maombi ya viza

Taarifa juu ya kuamza maombi yako

 • Wasilisha kwa kufika mwenyewe kwenye ofisini
 • Kuomba kwa njia ya posta
 • Kuomba kwenye mtandao
 • wasilisha pasipoti na nyaraka nyingine
 • Malipo ya huduma

Mwongozo wa hatua kwa hatua

Hatua za mchakato

 • Tambua aina ya visa

  Chagua viza sahihi kwa usafiri wako

  Hatua ya kwanza ni kuamua aina ya viza unayohitaji na kudhamini kama unakubalika kuomba.

  Pia utahitaji kujua hati unazopaswa kuwasilisha pamoja na ombi lako, muda ombi hilo litachukua na ada ya malipo.

  Kila ombi lahitaji kufwata mwongozo unaotumika kwa kitengo chake cha viza.

  Tembelea tovuti ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC) kwa mwongozo wa kina.

  Waweza kubonyeza vipengee vifuatavyo kwa taarifa ya kina:

  Viza ya muda mfupi

  Viza ya masomo

  Viza ya kazi

  Hati ya kusafiri ya wakazi wa muda mrefu

  Wahitajika kujaza na kutia sahihifomu ya ridhaa ya VFS na uambatanishe na fomu yako ya maombi.


 • Anzisha programu yako

  Anzisha ombi lako la viza

  Unaweza kupakua fomu ya ombi ya viza, uijaze, uchapishe fomu iliyo kamilishwa na uwasilishe kwa Kituo cha Maombi ya Visa. Unaweza pia kuwasilisha ombi lako mkondoni moja kwa moja kwa Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC).

  Jaza fomu ya ombi kwa njia ya kielektroniki. Yapaswa kuchapisha fomu iliyokamilishwa (ikiwemo kurasa ya baakodi) kwa karatasi nyeupe, ya ubora wa juu, isiyo telezi kwa kutumia printer ya laser. Tafadhali hakikisha kuwa baakodi imechapishwa wazi na kwenya karatasi ya ubora wa hali ya juu. Fomu iliyojazwa kwa mkono haikubaliki.

  YUtahitajika kuwasilisha viambatanishi vinavyohitajika kama ilivyotajwa kwenye Orodha ya nyaraka ya IRCC unaotumika kwa kila kitengo cha Viza. Kama hautaweza kuwasilisha viambatanishi vyote kama ilivyotajwa kwenye Orodha ya nyaraka zinazohitajika ya IRCC, utalazimika kujaza na kusaini Fomu maalum ya kutokuwa na viambatanisho na kisha ambatanisha na fomu yako ya maombi

  Soma sera ya faragha (Privacy policy) jaza fomu ya ridhaa ya CVAC na uambatanishe na fomu zako za maombi. Kama fomu ya ridhaa iliyojazwa na kuwekwa sahihi haijaambatanishwa na ombi lako, hatutaweza kukusaidia, na nyaraka zako za maombi zitarudishwa kwako


 • Kupanga apointmenti

  Chagua Kituo cha Maombi ya visa kisha uweke apointimenti

  Baada ya kukamilisha ombi lako, unahitajika kuweka miadiili alama za vidole na pichayako kuchukulia kwenya Kituo cha Maombi ya visa. Hii inajulikana kama usajili wa Biometriki.

  Baada ya kuhifadhi miadi, utapokea barua pepe na barua ya uthibitisho wa miadi uliyoomba.

  Ikiwa wewe ni sehemu ya familia au kikundi, itabidi uweke miadi ya kila mmoja wa familia au kikundi.

  Ikiwa hauhitajiki kusajili biometriki, hauitaji kufanya miadi ya kutembelea Kituo chako cha Maombi ya viza za Kanada. Waweza kutembelea Kituo cha maombi kwa wakati wako mwafaka ukiambatanisha na pasi, picha, fomu, ada ya malipo ya visa ya serkali ya Kanada, na viambatanisho kwenye orodha ya nyaraka ya IRCC.

  Ili kujua kama unahijatijika kusajili biometriki, tafadhali tembelea
  http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometrics.asp

 • Lipa ada yako

  Ufafanuzi wa ada ya malipo unayohitaji kulipa

  Unapomaliza ombi lako, utahitajika kulipa ada ya ombi lako la viza. Ikiwa umepakua fomu na kuiwasilisha kwa Kituo cha Maombi ya visa, utaweza lipa wakati wa apointimenti yako.

  YUtalazimika kulipa ada ya Serikali ya Canada na ada ya biometriki (ikiwa inahitajika) kulingana na maagiza kwenye tovuti ya IRCC kwenye ukrasa wa ada.

 • Tembelea Kituo cha Maombi ya viza

  Hudhuria miadi iliyopangwa

  Iwapo hutawasilisha ombi lank mkondoni, itakubidi uwasilishe fomu yako ya viza kwenya Kituo cha Maombi ya Viza.

  Ufafanuzi wa kinachoendelea kwenye Kituo cha Maombi ya Visa.

  Ikiwa hauhitaji kusajili biometriki, tafadhali tembelea Kituo cha Maombi ya visa wakati wowote kwa masaa ya kazi.

  Ukifika kwenya Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada, ombi lako la viza itachukulia na biometriki kusajiliwa. Lipa gharama ya huduma ya Kituo cha Maombi ya Viza na upewe risiti. Risiti hii itakuwa na nambari ya kipekee ya ombi lako itakayo kusaidia kufuatilia ombi hilo mkondoni.

 • Fatilia maombi yako

  Fahamu hali ya ombi lako

  YUtapokea sasisho la barua pepe wakati uamuzi wako umerejeshwa kwenya Kituo cha Maombi ya Viza. Ikiwa huwezi kupata barua pepe kwa urahisi, au ungependa maelezo ya kina, unaweza kupata visasisho kupitia kwa ujumbe mfupi utakao tumwa kwa simu yako. Thibitisha ikiwa huduma hii inapatikana kwenya Kituo cha Maombi ya viza unacho tembelea.

  Tembelea ukrasa  wa kufuatilia Ombi  ili kupata taarifa zaidi.

 • Kuchukua pasi yako

  Pokea pasipoti yako kutoka Kituo cha Maombi ya Visa

  Uamuzi wa ombi la viza unapokamilika, unaweza chukua hati zako kutoka Kituo cha Maombi ya viza binafasi au kutumia hati hizo kwa njia ya courier kwa gharama Zaidi. Thibitisha kwamba huduma hizo zinapeanwa na Kituo cha Maombi ya viza unachotembelea.

  Ndiposa uchukue majibu yako binafsi kutoka Kituo cha Maombi ya Viza, utahitajika kupeana:

  • Nakala ya ukurasa wa biografiki wa pasipoti yako
  • Risiti rasmi na asili iliyopeanwa na Kituo cha Maombi ya Viza
  • Kitambulisho rasmi cha serikali

  Umekubalika pia kutuma mjumbe kuchukua nyaraka ya uamuzi kutoka kwenye Kituo cha Maombi ya Viza. Mjumbe anahitajika kupeana:

  • Fomu ya huduma ya Kituo cha Maombi ya Viza iliyo na sahihi ya idhini,jina na uhusiano wa mjumbe na mwombaji.
  • Nakala ya ukurasa wa biografiki wa pasipoti ya mwombaji
  • Risiti rasmi na asili iliyopeanwa na Kituo cha Maombi ya Viza
  • Kitambulisho rasmi cha serikali cha mjumbe

  Ni jukumu lako kuangalia maelezo ya viza uliyopewa na kuhakikisha kuwa ni ya tarehe iliyopendekezwa kuingia Kanada, idadi ya viingilio vinavyohitajika na ya kusudi ya safari. Lazima uangalie maelezo haya punde tu unapopokezwa majibu yako. Kipindi cha uhalali na idadi ya maingizo imedhaminiwa na ofisi ya viza na inaweza tofautiana na ombi lako.

Je, uko tayari kufanya ombi?

Anzisha mchakato wa visa, kisha urejee VFS Global na nambari ya kummbukumbu kufaidika na huduma zinazotolewa.

Mwongozo wa hatua kwa hatua

Hatua za mchakato 

 • Tambua aina ya visa

  Chagua viza sahihi kwa usafiri wako

  Hatua ya kwanza ni kuamua aina ya viza unayohitaji na kudhamini kama unakubalika kuomba.

  Pia utahitaji kujua hati unazopaswa kuwasilisha pamoja na ombi lako, muda ombi hilo litachukua na ada ya malipo.

  Kila ombi lahitaji kufwata mwongozo unaotumika kwa kitengo chake cha viza.

  Tembelea tovuti ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC) kwa mwongozo wa kina.

  Waweza kubonyeza vipengee vifuatavyo kwa taarifa ya kina:

  Viza ya muda mfupi

  Viza ya masomo

  Viza ya kazi

  Hati ya kusafiri ya wakazi wa muda mrefu

  Wahitajika kujaza na kutia sahihifomu ya ridhaa ya VFS  na uambatanishe na fomu yako ya maombi.

   
 • Anzisha programu yako

  Anzisha ombi lako la viza

  Unapokuwa tayari kufanya ombi lako, utapakua fomu ya ombi na orodha ya viambatanishi husika kwa kitengo cha viza unayoomba. Jaza fomu ya ombi kwa njia ya kielektroniki. Yapaswa kuchapisha fomu iliyokamilishwa (ikiwemo kurasa ya baakodi) kwa karatasi nyeupe, ya ubora wa juu, isiyo telezi kwa kutumia printer ya laser. Tafadhali hakikisha kuwa baakodi aina ya 2D imechapishwa wazi na kwenya karatasi ya ubora wa hali ya juu. Fomu iliyojazwa kwa mkono haikubaliki.

  Utahitajika kuwasilisha viambatanishi vinavyohitajika kama ilivyotajwa kwenye Orodha ya nyaraka ya IRCC unaotumika kwa kila kitengo cha Viza. Kama hautaweza kuwasilisha viambatanishi vyote kama ilivyotajwa kwenye Orodha ya nyaraka zinazohitajika ya IRCC , utalazimika kujaza na kusaini Fomu maalum ya kutokuwa na viambatanisho, na kisha ambatanisha na fomu yako ya maombi. Iwapo utakosa kutoa hati kadri na orodha ya nyaraka ya IRCC, itasababisha kucheleshwa au kukataliwa kwa ombi lako la viza, idhini ya hati au hati ya usafiri.

  Somasera ya faragha jaza fomu ya ridhaa ya CVAC na uambatanishe na fomu zako za maombi. Kama fomu ya ridhaa iliyojazwa na kuwekwa sahihi haijaambatanishwa na ombi lako, hatutaweza kukusaidia, na nyaraka zako za maombi zitarudishwa kwako.

  IKama utachagua kutuma ombi lako kwa njia ya posta au courier, utapaswa kuweka vifwatavyo kwenye kifurushi cha ombi lako:

  1. Fomu husika iliyokamilika

  2. Orodha ya viambatanishi via ombi la kutumwa

  3. Hati za kuunga mkono na nakala ya ukrasa wa data kwenye pasi

  4. Thibitisho ya malipo ya ada ya serikali ya Kanada ikiwamo ada ya kusajili biometriki

  5. Ada ya malipo ya Kituo cha Maombi ya viza kupitia uhamisho kwa benki, pesa taslimu au kadi za malipo.

  Ikiwa unatuma ombi lako kwa Kituo cha Maombi ya viza, utahitaji kutumia chombo cha uhalisi wa biometriki kidhibitisha ikiwa unahitaji kusajili biometriki kwenya Kituo cha Maombi ya Viza.

  Unaweza tuma fomu zilizo kamilika na nyaraka za kuunga mkono kwenye bahasha iliyofungwa kwa anwani ifwatayo:

  Kituo cha Maombi cha Canada Visa
  Flr ya 5, jengo la Parkfield
  Njia ya Muthangari-Off Waiyaki, (Upinzani wa Safaricom Hse) Westlands
  Westlands, Nairobi,
  Kenya

  Ukipokea arifa ya usajili wa biometriki, utahitajika kuweka apointimenti na kuonekana ndani ya siku kumi za kazi kwenye Kituo cha Maombi ya visa ulichotumia ombi lako

 • Weka miadi

  Chagua Kituo cha Maombi ya visa kisha uweke apointimenti

  Baada ya kukamilisha ombi lako, unahitajika kuweka miadi ili alama za vidole na picha yako kuchukulia kwenya Kituo cha Maombi ya visa. Hii inajulikana kama usajili wa Biometriki.

  Baada ya kuhifadhi miadi, utapokea barua pepe na barua ya uthibitisho wa miadi uliyoomba. .

  Ikiwa wewe ni sehemu ya familia au kikundi, itabidi uweke miadi ya kila mmoja wa familia au kikundi.

 • Lipa ada yako

  Ufafanuzi wa ada ya malipo unayohitaji kulipa

  Unapomaliza ombi lako, utahitajika kulipa ada ya ombi lako la viza. Ikiwa umepakua fomu na kuiwasilisha kwa Kituo cha Maombi ya visa, utaweza lipa wakati wa apointimenti yako.

  Utalazimika kulipa ada ya Serikali ya Canada na ada ya biometriki (ikiwa inahitajika) kulingana na maagiza kwenye tovuti ya IRCC kwenye ukrasa wa ada na gharama ya huduma za VFS Global kulingana na maagizo kwa kipengee cha Malipo ya huduma.

 • Tembelea Kituo cha Maombi ya viza

  Hudhuria miadi iliyopangwa

  Utahitajika kuwasilisha fomu ya ombi la viza kwa njia ya posta au mjumbe wa courier

  Ufafanuzi juu kinacho endelea kwenye Kituo cha Maombi.

  Mchakato wa Kituo cha Maombi ya viza za Kanada kuhusu maombi yaliyotumwa :

  • Ombi la viza la kutumwa linapo pokelewa, Kituo cha Maombi ya Viza cha Kanada kitarekodi ombi hilo kwenya mtandao wa VFS Global, na nambari ya maalum ya kufuatilia ombi hilo itatolewa,
  • Barua pepe otomatiki itajisababisha, ikitoa nambari maalum ya kumbukumbu na ufatiliaji au kasoro yoyote kuhusiana na ombi hilo. Kituo kitawasiliana na muombaji kwa njia ya simu iwapo anwani ya barua pepe haiko.
  • Maombi ambayo hayaja kamilika yatawekwa pembeni na waombaji wata hitajika kupeana viambatanishi pungufu ndani ya siku kumi. Ombi hilolitaregeshwa kwako ikiwa utashindwa kulikamilisha ndani ya siku kumi.
  • Iwapo fomu au maelezo yake si sahihi au hayajakamilika, muombaji atastahili kutuma fomu sahihi na kamilifu ama kutumia huduma ziada ya kompyuta ya kujaza fomu iliyo kwenye Kituo cha Maombi ya Viza.
  • Iwapo hujalipa ada sahihi ya malipo ya serikali ya Kanada ikiwemo ada ya usajili wa biometriki (iwapo inahitajika), utahitajika kutuma dhibitisho ya risiti kwa Kituo cha Maombi ya viza ya ada sahihi ya malipo ya serikali ya Kanada itakayo kwa mtandao wa malipo wa IRCC.
  • Iwapo hujalipa ada sahihi ya huduma na huduma za ziada za Kituo cha Maombi ya Viza, utahitajika kutuma dhibitisho ya malipo hayo ilitumwa kupitia uhamisho kwa benki, pesa taslimu au kadi za malipo.
 • Fatilia maombi yako

  Fahamu hali ya ombi lako

  Utapokea barua pepe majibu ya ombi lako yatakapo rejeshwa kwa Kituo cha Maombi ya Viza. Unaweza pia kupata ujumbe mfupi kwa simu, iwapo huwezi kupata barua pepe kwa urahisi, au ungependa maelezo ya kina ya ufuatilizi. Angalia ikiwa huduma hii inapeanwa na Kituo cha Maombi ya Viza unachotembelea.

  YUtapokea arifu kupitia kwa barua pepe iliyo na nambari maalum ya kufuatilia ombi lako kwa muda wa siku mbili za kazi baada ya kupokea ombi lako.

  Unahitajika kufuatilia ombi lako la kutumia kupitia kampuni uliyo tumia kuwasilisha ombi kwa Kituo cha Maombi cha Kanada.

  Tembelea ukrasa wa kufuatilia Ombi ili kupata taarifa zaidi.

 • Kuchukua pasi yako

  Pokea pasi yako kutoka kwa Kituo cha Maombi ya viza

  Baada ya uamuzi wa ombi la viza, muombaji atachukua nyaraka ya majibu kutoka Kituo cha Maombi ya viza au kutumia huduma ya courier kwa gharama zaidi.

  Kuchukua majibu yako binafsi: Utahitajika kuleta Risiti rasmi na asili iliyopeanwana Kituo cha Maombi ya Viza pamoja na kitambulisho rasmi cha serikali.Umekubalika pia kutuma mjumbe kuchukua nyaraka ya uamuzi kutoka kwenye Kituo cha Maombi ya Viza. Atahitajika kupeana barua iliyo na sahihi ya idhini yako, risiti rasmi na asili iliyopeanwa na Kituo cha Maombi ya Viza na kitambulisho rasmi cha serikalicha mjumbe.

  Tafadhali wasiliana na Kituo cha Maombi cha Visa wakati wa miadi yako kwa chaguzi zinazopatikana kukusanya hati zako.

  Iwapo utachukua majibu yako binafsi au kupitia kwa mwakilishi halali, utapokea barua pepe kukuarifu kuchukua nyaraka kutoka Kituo cha Visa cha Kanada.

Je, uko tayari kufanya ombi?

Anzisha mchakato wa visa, kisha urejee VFS Global na nambari ya kummbukumbu kufaidika na huduma zinazotolewa.

Mwongozo wa hatua kwa hatua

Hatua za mchakato

 • Tambua aina ya visa

  Chagua viza sahihi kwa usafiri wako

  Hatua ya kwanza ni kuamua aina ya viza unayohitaji na kudhamini kama unakubalika kuomba.

  Pia utahitaji kujua hati unazopaswa kuwasilisha pamoja na ombi lako, muda ombi hilo litachukua na ada ya malipo..

  Kila ombi lahitaji kufwata mwongozo unaotumika kwa kitengo chake cha viza.

  Tembelea tovuti ya Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC) kwa mwongozo wa kina.

  Waweza kubonyeza vipengee vifuatavyo kwa taarifa ya kina:

  Viza ya muda mfupi

  Viza ya masomo

  Viza ya kazi

  Hati ya kusafiri ya wakazi wa muda mrefu

  Wahitajika kujaza na kutia sahihifomu ya ridhaa ya CVAC  na uambatanishe na fomu yako ya maombi.

   
   
 • Anzisha programu yako

  Anzisha ombi lako la viza

  Unaweza pia kuomba mkondoni, kwa kujaza fomu ya maombi ya visa.

 • Weka miadi

  Chagua Kituo cha Maombi ya viza kisha uweke miadi

  Unapo maliza kuweka ombi lako la viza, utahitajika kuweka apointimenti ya kuchukuliwa vidole na picha kwenya Kituo cha Maombi ya viza. Kwa vinginevyo kama bayometriki..

  Baada ya kuhifadhi miadi, utapokea barua pepe na barua ya uthibitisho wa miadi uliyoomba.

  Ikiwa wewe ni sehemu ya familia au kikundi, itabidi uweke miadi ya kila mmoja wa familia au kikundi.

  Barua ya miadi itakuwa na nambari maalum ya kumbukumbu na maelezo ya tarehe, wakati na pahali pa apointmenti na taarifa yote husika.

  Iwapo hautaji kusajili bayometriki, utangojea jibu la ombi lako na kufuatilia kupitia kwa akaunti yako ya MyCIC kwa maagizo zaidi.

  Iwapo utahitajika kusajili bayometriki baada ya ombi mtandaoni, utapokea arifu kupitia kwa barua ya maagizo ya kusajili bayometriki (BIL). Unapopokea barua hii, utahitaji kutembelea Kituo cha Maombi ya Viza kwa ajili ya bayometriki.

 • Lipa ada yako

  Unapomaliza ombi lako, utahitajika kulipa ada ya ombi lako la viza


  Unapomaliza ombi lako, utahitajika kulipa ada ya ombi lako la viza.

  YUtalazimika kulipa ada ya Serikali ya Canada ikiwemo biometriki (ikiwa inahitajika) kulingana na maagiza kwenye tovuti ya IRCC.

 • Tembelea Kituo cha Maombi ya viza

  Hudhuria miadi iliyopangwa

  Utaweza kuwasilisha ombi lako kamilifu mtandaoni.

  Ufafanuzi juu ya kinacho endelea kwenye Kituo cha Maombi.

  Baada ya usajili wa bayometriki, utapokea risiti thibitishi kwa bayometriki yako imechukuliwa na Kituo cha Maombi ya Viza.

  Uamuzi wa ombi lako la viza utakapo kamilika, utajuzwa kwa barua pepe kuwasilisha passport kupitia kwa barua ya ombi la pasipoti. Iwapo una shauku ya kupokea barua pepe kutoka IRCC, tafadhali angalia akaunti yako ya MyCIC kwa sasisho.

  Unapopokea barua ya ombi la pasipoti, utahitajika kuwasilisha pasipoti asili na barua ya ombi la pasipoti kwa Kituo cha Maombi ya Visa.

  Kwa muongozo kamili juu ya kuwasilihsa pasipoti na nyaraka zingine zinazounga mkono, tafadhali tazama kipengee kilicho juu ya ukrasa huu.

Je, uko tayari kufanya ombi?

Anza mchakato wa maombi yako ya viza na kisha rudi tena VFS Global na namba yako ya kumbukumbu ili ufaidike na huduma zinazotolewa.

wasilisha pasipoti na nyaraka nyingine

Uliweka ombi mtandaoni yaani E-app au:

 1. Uliweka ombi mtandaoni yaani E-app au;
 2. Utahitajika kulipa ada ya kusafirisha kifurushi ukiwasilisha nyaraka za ziada na pasi kwa Kituo cha Maombi ya viza. Ikiwa sivyo, unatakiwa kuwasilisha pasi yako ya kusafiria (Pasipoti) kwenye kituo cha maombi ya viza ambapo ulitoa alama zako za bayometriki na huja wasilisha nyaraka au pasi awal.

Utahitajika kulipa ada ya kusafirisha kifurushi ukiwasilisha nyaraka za ziada na pasi kwa Kituo cha Maombi ya viza. Ikiwa sivyo, unatakiwa kuwasilisha pasi yako ya kusafiria (Pasipoti) kwenye kituo cha maombi ya viza ambapo ulitoa alama zako za bayometriki na huja wasilisha nyaraka au pasi awal.

Wahitajika kujaza na kutia sahihi fomu ya ridhaa ya VFS Global iwapo unahitaji huduma zaidi kutoka Kituo cha Maombi ya Viza.

 1. Iwapo utatuma nyaraka au/na pasi kwa Kituo cha Maombi ya Viza za Canada bila malipo ya ada ya kusafirisha kifurushi na Fomu ya ridhaa ya VFS, kifurushi cha ombi kitazingatiwa kuwa hakijakamilika. Utalazimika kulipa ada ya malipo ya kusafirisha kifurushi kwa muda wa siku kumi za kazi. Kifurushi hiki kitregeshawa kwako kwa kukosa kulipo malipo hayo kwa siku kumi.
 2. Binafsi – utahitaji kuleta pasipoti asili ikiambatana na barua ya ombi la pasi kwa Kituo cha Maombi ya Viza. Utahitajika kulipa ada ya malipo ya usafirishi wa kifurushi unapo wasilisha pasi yako.
 3. Kupitia kwa mwakilishi aliyeidhinishwa - utahitaji kuleta pasipoti asili, ikiambatana na barua ya ombi la pasi, na Fomu ya ridhaa ya VFS Global iliyo na sahihi ya kuidhinisha mwakilishi kwa Kituo cha Maombi ya Viza. Utahitajika kulipa ada ya malipo ya usafirishi wa kifurushi unapo wasilisha pasi yako.

  Kwa Maelezo kamili juu ya gharama za huduma ya Kituo cha Maombi, tafadhali bonyeza kipengee cha gharama ya malipo iliyo juu ya ukrasa huu.

  IIwapo wewe ni muombaji wa makazi ya kudumu na ombi lako limekamilika, utapokea ushauri wa kuwasilisha pasi yako,  picha kulingana na mashauri yaliyo wekwa na IRCC na kiambatanisho B kilicho kamilika. Angazia ushauri uliyotumia kujaza taarifa na maagizo. Kuwasilisha pasi yako inahitaji malipo ya ada ya usafirishi wa kifurusha kwa Kituo cha Maombi ya Viza.

  Unapokamilisha mchakato wa kuwasilisha pasi yako, utapewa risiti itakayo onyesha malipo kwa jumla sawiya na huduma ziada ulizotumia kwa Kituo kwa Maombi ya Viza. ICR vilevile itakuwa na nambari ya kumbukumbu ya ombi lako utakayotumia kufuatilia ombi mtandaoni.

  Pasi itakaporudishwa kutoka Ofisi ya Viza Kanada hadi Kituo cha Maombi ya Visa, unaweza:

  1. Kuchukua pasi yako binafsi kutoka Kituo cha Maombi ya Viza Utahitajika kuleta kitambulisho chako cha serikali na risiti asili iliyopewa na Kituo cha Maombi ya Viza.
  2. Umekubalika pia kutuma mjumbe au mwakilishi kuchukua pasi yako. Atahitajika kupeana Fomu ya ridhaa ya VFS Global iliyo na sahihi ya idhini yako, kitambulisho chako cha serikali cha mwakilishi, kitambulisho chako cha serikali na risiti rasmi na asili iliyopeanwa na Kituo cha Maombi wakati wa kuwakilisha ombi;
  3. Iwapo unahitaji pasi yako kupelekwa kwa eneo unalopena, unaweza kuangalia huduma ziada zinazotolewa na Kituo Cha Maombi cha Viza kilicho karibu.

Gharama za Huduma

gharama za huduma zitakazoanza kutumika tarehe 02 Novemba, 2019

Iwapo utahitaji kutoa alama za vidole na picha, gharama yake itakuwa ni dola 85 za Canada (Kwa mtu mmoja) / dola 170 za Canada (kwa familia ya watu wawili na zaidi) / dola 255 za Canada (kwa kikundi cha wasanii watuta na zaidi) ambayo itajumuisha gharama za huduma za kusafirisha Kifurushi za Kituo cha maombi ya Viza. Usafirishi wowote wa pasi na/ au nyaraka baada ya usafirishi wa awali, waombaji watahitajika kulipa ada ya usafirishi wa kifurushi.

Waombaji wote ambao wanawasilisha maombi ya karatasi (iliyo au bila bayometriki) watahitaji kulipa huduma ya usaidizi- ada ya ombi la kartasi

Iwapo unahitaji kusajili bayometriki na kuwakilisha pasi na/au nyaraka kwa Kituo cha Maombi ya Viza, ada ya malipo ya usafirishi wa kifurushi itatumika.

Njia za kulipa

Ni lazima kuwa ada ya malipo ya serikali ya Kanada hulipwa mtandaoni. Ukitaka ufafanuzi jinsi ya kulipa ada ya malipo ya serkiali ya Kanada tembelea ukrasa wa ada ya malipowa IRCC.

Maelekezo kuhusu malipo ya gharama za huduma za Kituo cha Maombi ya Viza na huduma za hiari

 • Binafsi – Kupitia Mpesa
 • Ombi la kutumwa na Courier/posta – - YAda inaweza kulipwa kwa uhamisho kwa benki kwa "VFS Kenya Limited" kwa shilingi ya Kenya tu.

  Ufuatao ni muongoza wa malipo ya uhamisho kwa benki

  Akaunti ya VFS Global Kenya limited

  Jina la akaunti: VFS (Kenya) Limited- Canada Holdings Nchi: Kenya Fedha: Kenya Shilling Jina la Benki: Barclays Bank Tawi: Barclays Plaza Mtaa: Loita Street - Nairobi Nambari ya akaunti. 2037342214 Nambari ya IBAN. 2037342214 Nambari ya SWIFT: BARCKENX Nambari ya Chips UID/Sort code: 03

  Correspondence bank account details

  Benki ya mawasiliano: Barclays New York Jiji/mtaa: New York Nchi: USA Nambari SWIFT: BARCUS33

Kwa urejeshwaji wowote wa ada iliyolipwa kwa Serikali ya Canada bonyeza hapa kuomba marejesho kutoka kwa Serikali ya Canada.

Malipo ya Huduma kwa Huduma inayotolewa katika VAC:

Gharama za Huduma (kwa kila muombaji)

Kiasi kwa C$ (Pamoja na VAT)

Kiasi kwa Shilingi (Pamoja na VAT)

Kutuma Kifurushi (Bei kwa kila kifurushi)

$24.67

1,910.00

Huduma za usaidizi – Fomu kwa mtandao (Bei kwa kila fomu)

$2.00

155.00

Huduma za usaidizi – Maombi ya karatasi (Bei kwa Ombi)

$7.95

615.00

Huduma za usaidizi – Skanning (Bei kwa kila ukurasa)

$0.28

20.00

Huduma ya kompyuta unayoitumia binafsi (Bei kwa saa)

$5.09

395.00

Garama za Courier kutuma njia moja (Kila kifurushi) -Nairobi

$6.97

540.00

Garama za Courier kutuma njia moja (Kila kifurushi) – Inje ya Nairobi

$13.83

1070.00

Huduma za kurudufu (Bei kwa kila ukurasa)

$0.08

5.00

Kuchapa nyaraka (Bei kwa kila ukurasa)

$0.50

40.00

Picha inayokubalika kwa kiwango cha shirika la International civil Aviation (ICAO)

$8.43

655.00

Ujumbe mfupi “kwa kila ombi”

$2.75

215.00

 

*Malipo ya huduma yanajumuisha ushuru wowote unaotumika na yanabadilishwa kulingana na arifa ya serikali.

**Kiwango cha ubadilishaji wa CAD kimedhamiriwa na serikali ya Canada.

Malipo mapya ya huduma yakaanza kutumika mnamo Novemba 2, 2019. Tarehe ya uwasilishaji ya maombi ya courier au posta itakuwa tarehe ambayo Kituo cha Maombi cha Visa kinapokea maombi. Ikiwa maombi ya kutumwa na courier au posta yamepokelewa na hayakujumuisha malipo sahihi kwa malipo ya huduma ya sasa, mwombaji atawasiliana ili kulipa tofauti hiyo au maombi yatarudishwa kwa mwombaji.

Kwa maelezo kamili juu ya huduma za ziada zinazotolewa katika Kituo cha Maombi ya Visa, tafadhali bonyeza hapa.

Je, ushafanya ombi lako la viza?

Kingine unachoweza kufanya ni hiki

Weka miadi

Kuweka Apointimenti nasi

Fatilia maombi yako

Fahamu hali ya ombi lako

Tafuta kituo

Taarifa ya kituo cha karibu

Nunua huduma

Furahia ombi la haraka, bila usumbufu na lenye starehe