Kutuhusu

Je, Sisi ni nani?

Kwa sababu ya mkataba uliotolewa na Serikali ya Kanada, VFS Global itatoa huduma za msaada kwa maombi ya viza za Kanada kupitia Vituo vya Maombi vya Mamombi ya Viza za Kanada

Vituo vya Maombi ya Visa za Canada ulimwenguni vitaongezaa ufikiaji wa huduma bora za kiutawala kwa waombaji kupitia njia thabiti ya utoaji wa huduma, ambayo pia itasaidia ukusanyaji wa bayometriki.

Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada kitatoa huduma ya kipekee kwa Serikali ya Kanada, na kuidhinishwa kukubali maombi ya aina zote za makazi ya muda (viza za wageni, viza za kusoma na vibali vya kufanya kazi) na maombi ya hati ya kusafiri kutoka ya wakaazi wa kudumu wa Kanada nchini Nairobi

Kituo cha Maombi ya Visa za Kanada kimepewa dhamana ya kutoa huduma za usaidizi wa kiutawala, kama vile miadi ya kupanga, kukusanya maombi ya visa, kusajili bayometriki na kurudisha pasi katika bahasha za uamuzi zilizo na fungwa kwa waombaji.

Kituo cha Maombi ya Viza hutoa tu habari ya jumla na huduma za kiutawala zinazohusiana na maombi ya wakaazi wa muda, pamoja na vibali vya kusoma na kazi, na vile vile hati za kusafiri kwa wakaazi wa kudumu wa Kanada. Vituo vya Maombi ya Visa haviruhusiwi kutoa habari yoyote, au kujibu maswali yoyote, kuhusu maombi ya makazi ya kudumu na huduma za wakala wa Kanada. Hii ni pamoja na Uingilio wa Express kwa wahamiaji wenye ujuzi, msaada wa maombi ya mkondoni, uraia wa Canada na habari yoyote maalum kuhusu fomu za maombi ya visa, nyaraka zinazounga mkono au ushauri wowote unaohusiana na mchakato wa maombi ya visa. Tafadhali tembelea tovuti ya Uhamiaji, wakimbizi na uraia Kanada (IRCC) kwa habari zaidi juu ya programu hizi.

Uamuzi wa kutoa au kukataa kutoa viza unafanywa na maafisa wa Uhamiaji, Ukimbizi na Uraia Kanada (IRCC) pekee na maombi yote yatatathiminiwa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya viza za uhamiaji Kanada. Tafadhali kumbuka kuwa VFS Global ikiwa CVAC sio enjeti wala waakilishi wa serikali ya Kanada. CVAC haina jukumu wala ushawishi wa matokeo ya maombi ya viza na haitatoa ushauri wowote wa kitathimini.

Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea vfsglobal.com

Onyo la juu ya Uhamiaji!

Jihadhari Na Kazi Za Ulaghai. Kwa taarifa zaidi, bonyeza hapa

Nani anaamua kama nitapata Viza?

Maombi yako ya viza yatafanyiwa kazi na Serikali ya Kanada, ambayo itafanya maamuzi yote kuhusiana na maombi yako ya viza. VFS Global na wafanyakazi wake hawana mchango wowote au ushawishi wowote katika matokeo ya maombi yako. VFS Global wanaweza tu kutoa huduma kuhakikisha kwamba maombi yako ya viza yamejazwa vizuri na yamewasilishwa.