Karibu VFS Global

VFS Global ni mtoa huduma maalumu kwa serikali ya Kanada, aliyeidhinishwa kutoa huduma za kiutawala kwa wanaoomba viza nchini Nairobi

Fanya maombi ya viza

Pata taarifa na uanze ombi lako

Weka miadi

Kuweka Apointimenti nasi

Tafuta kituo

Taarifa ya kituo cha karibu

Nunua huduma

Furahia ombi la haraka, bila usumbufu na lenye starehe

Taarifa muhimu

 • Kituo cha Maombi ya visa cha Nairobi kitafunguliwa Jumatano 09 Septemba na kutoa huduma zifuatazo kwa muda usio julikana:

  • Kusajili biometriki kwa wale walio na barua ya maagizo ya baiyometriki (BIL)

  • Kuregesha bahasha za uamuzi kwa waombaji: Bahasha iliyo na uamuzi wa ombi la viza iteregeshwa kupitia kwa huduma ya courier inayotolewa na Kituo. Kuchukua hati hizi binafsi kumepigwa marufuku kwa muda usiojulikana. Tazama ukrasa wa “Nunua Huduma” kwa tovuti hii kwa maelezo kamili juu ya huduma ya courier inayotolewa na kituo cha maombi ya Viza za Kanada.

  • Hati za kusafiri za wakazi wa muda mrefu zitatumwa kwa njia ya posta au courier: Kuwasilisha Maombi ya hati za kusafiri za wakazi wa muda mrefu kibinafsi umesitishwa kwa muda usio julikana

  • Kuwasilisha pasi baada ya kupokea ushauri wa Uhamiaji wakimbizi na Uraia Canada ni kwa njia ya posta au courier. Kuwasilisha pasi kibinafsi kwa kituo cha Maombi ya visa umesitishwa kwa muda usio julikana

  Masaa ya kufungua kituo cha maombi ya viza yatakuwa ifuatavyo kwa muda usio julikana:

  • Masaa ya kazi: Jumatatu na Jumatano (Siku mbili pekee) 08:00 hadi 15:00

  Kufuatana na mkurupuko wa Covid 19, kituo cha maombi ya viza kitatekeleza hatua za kuimarisha afya na usalama wa wateja.

 • MUHIMU

  Kufuatia maagizo ya wizara yaliyotolewa na Waziri wa uraia na uhamiaji wa Kanada mnamo tarehe 9 Aprili, 29 Aprili, 19 Mei, 09 Juni na 01 Julai 2020, waombaji wote hawatoweza kuwasilisha maombi yao ya viza ya muda mfupi kwa njia ya karatasi kwenye kituo cha maombi ya viza. Maagizo mapya ya Waziri yaliyotolea Tarehe 01 Julai 2020 yataendelea hadi tarehe 30 Septemba 2020. Waombaji wote wa visa ya muda mfupi wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya IRCC :https://www.canada.ca/en/services/immigration-citizenship.html

  Kama uliwasilisha maombi ya visa ya muda mfupi kwa njia ya karatasi kwenye kituo cha maombi ya viza ya Kanada mnamo au baada ya tarehe 10, Aprili 2020, maombi yako yatarudishwa kwako.

  Tafadhali tambua kuwa kuanzia tarehe 1 Julai, Waziri wa Uraia na Uhamiaji wa Kanada, pia ameondoa zuio kwenye mchakato wa maombi ya Viza za makazi ya muda mfupi (Viza ya matembezi). Ingawa mchakato wa maombi umerudi kama mwanzo, vikwazo vya kuingia Kanada bado vinaendelea. Kwa Maelezo Zaidi tembelea tovuti ya IRCC.

 • Kituo cha Maombi ya viza Nairobi kitafungwa Jumanne 11 Februari 2020 kwa ajili ya ibada ya kumbumbu kufwatia kifo cha rais wa pili wa jamhuri ya Kenya. Huduma za kawaida zitarejea Jumatano 12 Februari 2020
 • 08 August 2019
  Kuweka miadi ya kuchukuliwa alama za vidole na picha (biometriki) ni lazima